1. Uzima ninao moyoni kweli,Uzima huo ni Yesu.
Aliyeingia rohoni mwangu, Akanitia imani.
Nashiba rohoni kwa raha yake, Ninao
moto wa Mungu. Naishi katika nuru
kabisa, Na nuru hiyo ni Yesu.
2. Nilipoziungama dhambi zangu Kwa
Yesu Mwokozi wangu. Baraka zilizo
katika Yeye Nilizipokea bure.
3. Yesu aliniondoa gizani, Natunzwa nuruni
mwake, Na sasa kwa nguvu zake
Mwokozi, Namtumikia Yeye.
4. Ninayo maisha yenye maana,
Nam-tumikia Yesu. Kuishi ni Kristo,
Kufa faida, Nikiwa Mkristo kweli.
Comments
Post a Comment