- Mungu, washa moto wako kwangu,
Ninangoja nguvu yako. Nipe uzima na
pendo lako, Unijaze, ee Mwokozi wangu! - Teketeza usiyoyapenda, unisafishe
kwa damu. Na kiburi changu ukivunje,
Unioshe Yesu, niwe safi! - Unilinde Yesu, nisiasi, Unifunge
kwa upendo. Mimi ni dhaifu, unitunze,
Niongoze kwa m-kono wako! - Huko mbinguni tutafurahi, Na huzuni
zitakwisha. Nyimbo zitaimbwa za kusifu;
Utukuzwe, Yesu, Mkombozi!
Comments
Post a Comment