1. Nataka kupokea baraka za Mungu,
Nibatizwe katika Roho Mtakatifu,
Ahadi yake Mungu inanipa raha,
Nangoja kwa imani ataitimiza.
Kama bahari, Kama bahari,
Neema ya Mungu katika Yesu,
Anayenijaza na kuniponyesha,
Asifiwe sana, Mwokozi wangu!
2. Kanisa la Mungu linanyeshewa mvua,
Vijito vya baraka vinamiminika.
Furaha ya uzima yatufurukia.
Tuimbe Haleluya! Tumsifu Yesu!
3. Mawimbi ya wokovu yanatufikia.
Ee Mungu tunaomba: Nasi utujaze!
Twataka kutakaswa sisi watu wako!
Tuimbe Haleluya! Tumsifu Yesu!
4. Mawimbi ya wokovu yaliyotujia,
Ee Mungu uyatume pote duniani,
Maelfu na maelfu wapate wokovu,
Waimbe Haleluya Wamsifu Yesu!
Comments
Post a Comment