151 MWOKOZI TUMA MOTO WAKO


1. Mwokozi tuma moto wako, Ulioahidi zamani!
Twaomba kwako leo Mungu:Washa moto huo
moyoni! Tazama sisi hapa leo, Tupe Roho wako
Mungu!Tupate Pentekoste yetu, Tuma moto
wako juu yetu!


2. Ee Mungu wetu usikie, Tuma moto wako
juu yetu! Twadumu katika kuomba: Washa
moto wako moyoni! Tunahitaji nguvu yako,
Tupate kutakasika, Na kuyashinda majaribu,
Tuma moto wako juu yetu!


3. Mioyo iliyo baridi, Yahitaji moto toka juu.
Hitaji zote tutajazwa, Tukipata moto
mioyoni. Siwezi mimi peke yangu,
Kuyashinda majaribu, Lakini nakuomba
Mungu: Washa moto wako moyoni.


4. Naomba moto juu yangu, Ili nihudumu kwa
pendo! Nauhitaji moto wako, Niwe nazo nguvu
na bidii. Juu ya madhabahu takatifu, Nauweka
moyo wangu. Juu ya sadaka yangu Mungu,
Washa moto wako naomba.


Comments