1. Usimtafute Yesu Kaburini kwa wafu!
Alikufa kwa hakika, Lakini ’kafufuka.
:/:Yesu Mwokozi yu hai! Alishinda mauti!:/:
2. Aliwekwa kaburini, Ukatiwa muhuri,
Lakini alifufuka, Yu hai, Tufurahi!
:/:Yesu Mwokoziyu hai! Tufurahi po pote!:/:
3. Bwana Yesu ’kafufuka! Habari zienezwe!
Yu Mwokozi wetu kweli, Aliyetufilia,
:/:Yesu Mwokozi yu hai! Asifiwe daima!:/:
Comments
Post a Comment