155 KATIKA TUMAINI


1. Katika tumaini, Kwa Mungu wangu Naishi kwa
Amani na utulivu,Yeye ni mwamba wangu,
Imara sana, Katika mambo yote, Ananilinda.


2. Jina la Yesu Kristo Ni ngome yangu, Ni
Kimbilio langu nyakati zote. Katika vita kali
Sitaogopa, Msaidizi wangu Akiwa nami.


3. Mahali pa amani, Mwamba wa kale,
Ninastarehe, Kwako nimejificha, Na pepo
Zikivuma, Sitaogopa, Napata raha kwako Katika mwamba.


Comments