158 HERI MTU AMWAMINIYE


1  Heri mtu amwaminiye Mungu Baba
Na Yesu Bwana! Heri atakayefuata
Njia iendayo mbinguni.


Tumsifu Mwokozi Kwa wokovu tuliopewa!
Tumsifu Mwokozi, Tutamwona kwake mbinguni!



2. Kwa furaha twakusanyika
Kusikia Neno la Mungu. Mbinguni
Karibu na Yesu Tutashangilia milele.


3. Ni heri kumwamini Yesu
Ingawaje hatujamwona. Siku moja
Atatuita, Tuingie kwake mbinguni.


Comments