- Yo yote uyaonayo safarini mwako,
Yafaa kumwamini Yesu, Atakusaidia
Kwa kuwa anayemwomba Mungu Baba
yetu, Aokoka hatiani, Na atamsifu Yesu. - Ukichukiwa na watu, Na ukijaribiwa,
Mwokozi yu karibu, Na maombi asikia. - Ikiwa umepotea, Uko mbali na Mungu,
Na amani unakosa, Urudi kwake Yesu. - Ukiwa na makosa, Na roho yako ni ngumu,
Neema yake yakutosha, utubu dhambi zako. - Ukiwa na udhaifu, Kuomba kwa bidii,
Uombe kama m-toto, Akusikia kweli.
Comments
Post a Comment