1. Ahadi zote za Mungu wetu Zinasimama Hata milele. Milima yote ikianguka, Ahadi zinadumu.
Ahadi zake zinasimama, Zinadumu hata milele. Ikiwa nyota zingezimika, Ahadi zake zadumu.
2. Ahadi zake zinasimama Katika shida, Katika giza. Na nikichoka kwa vita kali, Ahadi zinadumu
3. Ahadi zake zinasimama Katika homa Katika kufa. Nafarijiwa na Baba yangu, Ahadi zinadumu.
4. Ahadi zake zinasimama; Nitaamshwa Kutoka wafu. Kwa Baba nitapokea taji, Ahadi zinadumu.
Comments
Post a Comment