161 UMESHIRIKIANA NAYE YESU


1. Umeshirikiana naye Yesu, Kama tawi
Ndani ya mzabibu? Una raha iliyo timilifu,
Umejazwa Roho Mtakatifu?


Umeshirikiana naye Yesu Kama tawi ndani ya
mzabibu? Kuna raha na nguvu Unapomwomba
Mungu, Akutia nguvu ili ushinde.


2. Umepata imani ishindayo Katika mashaka
Na shida huku? Umepata neema ya kudumu,
Inayokulinda katika yote?


3. Kwa Yesu ni mahali pa amani, Hapo ndipo
Pa Kuburudikia. Atujaza mioyo utulivu
Ili tuwe na amani daima.


4. Twafurahi kwa wema wake wote,
Tunashukuru kwa ulinzi wake. Hata
Tukiudhiwa huku chini, Atatufikisha kwake
Huko juu.

Comments