1. Ahadi zote za Mungu Zasimama kweli
Na zilitiwa muhuri kwa damu ya Yesu.
Mbingu zikiondoka, Nchi ikitoweka,
Kwao wamwaminio Ahadi zadumu.
2. Fanya kama Ibrahimu, Uangalie juu!
Nyota ukizihesabu, Imani huzidi.
3. Katika giza njiani Tutaamini tu.
Muda kitambo, na tena Jua lita-angaa.
4. Watu wakitusumbua, Tutaamini tu.
Yesu atusaidia, Tukijaribiwa.
5. Rafiki wakituacha, Tutaamini tu.
Yesu, Rafiki wa kweli, Hubaki daima.
6. Na katika mambo yote, Tutaamini tu.
Tutaviona mbinguni Tulivyoamini.
Comments
Post a Comment