164 WANA WA ISRAELI ZAMANI


1. Wana wa Israeli zamani, Wazunguka
Mji wa Yeriko. Mwenyezi Mungu .
Aliwaongoza, Kwa imani yao walishinda.


Nasi tushinde, Nasi tushinde!
Kwa damu ya Yesu nasi tushinde!
Tumwamini Mungu Atuongoze
Na sisi kwa imani twashinda .


2. Daudi, mchungaji, ’kaenda kupigana
Naye Goliathi. Kwa imani alilitupa jiwe,
Kwa jina la Mungu akashinda.


3. Danieli kaomba daima, Hakulihofu
Pango la simba. Alipomwomba Mungu
Kwa imani, Akaokoka kwenye hatari.


4. Katika safari ya mbinguni, Sina budi
Kupita jangwani. Nikipatwa na majaribu
Mengi, Ushindi ninao kwa imani.


5. Imani hum-shinda Shetani, Na mambo
Yake yote ya giza. Niliye dhaifu .
Sitaogopa, Kwa kuwa Mungu aniokoa.


Comments