165 NIKIMTAZAMA MWOKOZI


1. Nikimtazama Mwokozi, Sivutwi tena na
Dhambi, Nauona utajiri Wa Mungu wetu
Mbinguni. Haleluya, furaha kuu, Atubeba
Kila siku. Hata tukiwa dhaifu, Yesu ndiye
Nguvu yetu.


2. Mungu akiwako nami Ndipo nitashinda
Dhambi. Aniongoza njiani, Nifike kwake
Mbinguni. Haleluya, Mungu wangu Asikia
Ombi langu. Hata wewe utamwona Kama
Ukimtafuta.


3. Nilipokuwa dhambini Niliteseka rohoni,
Lakini nilipotubu Nilipokea wokovu. Haleluya,
Ananipa Nguvu yake ya Kushinda. Mimi si
mtumwa tena, Yesu amenikomboa.


4. Haidhuru kuudhiwa Na hata
Kudhihakiwa. Nina urithi mbinguni
Na Mungu ni Baba yangu. Haleluya,
Mungu wangu Ananitunza daima. Nikiwa
Na udhaifu Natiwa nguvu na Mungu.

Comments