1. Tukimpenda Mungu na kushika Neno,
Tutapata raha moyoni. Tukim-pendeza .
Kwa matendo yetu, Yeye yupo nasi njiani.
Amini tu, Umtii Mungu, Utapata
furaha na raha moyoni.
2. Katika dhoruba na mawimbi mengi,
Neno la Yesu hutuliza. Kama tukikuta
Majaribu mengi, Ushindi upo kwake Yesu.
3. Mambo ya dunia yakitulemea ,
Tunapum-zishwa na Yesu. Masumbuko yote
Yatoka kabisa, Kwa kutii Neno la Mungu.
4. Tuna raha kubwa kwenye mashindano
Kwa kutii Neno la Mungu. Jua la upendo
Linawaangaza, Wenye kuamini na kutii.
Comments
Post a Comment