1. Namjua rafiki mwema, Anitunza vema
Daima. Aniponya maradhi, Ayafuta
Machozi. Jina lake ni Yesu Kristo.
Namjua Rafiki mwema, Na Yeye ajaa
neema. Ombi alisikia Na kunitegemeza.
Ndiye Yesu, na si mwingine.
2. Nimepata Rafiki mwema, Anifariji roho
Yangu. Nikim-tegemea Sitaogopa tena,
Rafiki ndiye Yesu Kristo.
3. Nifikapo mtoni pale Paitwapo "kufa"
Na "mtengo", Sitafadhaika la, Yesu
Yupo daima. Ni rafiki yangu wa kweli.
4. Pwani nzuri ya huko juu Nifikapo kwa
Neema kuu, Nitam-sifu Yesu, Ndiye
Mwana wa Mungu, Kwa ajili ya pendo lake.
Comments
Post a Comment