168 NINA FURAHA NA USHIRIKA


1. Nina furaha na ushirika Nikimtegemea
Mwokozi. Waaminio wana uheri
Kustarehe katika Yesu.


Raha, raha, Raha kwa Yesu daima.
Raha, raha, Nastarehe katika Yesu.


2. Raha ya kweli rohoni mwangu,
Nikimtegemea Mwokozi. Neno la Mungu
Ni nuru yangu, Nastarehe katika Yesu.


3. Woga, huzuni zinaondoka,
Nikimtegemea Mwokozi. Nafarijiwa
Moyoni mwangu, Nastarehe katika Yesu.

Comments