1. Sisi askari wa Mungu, Kwa shangwe
Twasonga mbele, Japo vita ni kali
Tuna nguvu na bidii. Tuna upanga wa Roho,
Ni Neno la Mungu wetu, Na kwa jina
Lake Yesu Twashangilia sana.
Mbio tutaondoka Vita ikiisha.
Tutakwenda mbinguni na kustarehe.
Wote wanaoshinda Watapokea Taji ya
utukufu ’toka kwa Mungu.
2. Na kila mtu avae Silaha zote za Mungu.
Mishale ya Shetani Itazimishwa kweli.
Tukimtii Mwokozi, Twaendelea kwa bidii,
Na kwa nguvu za ahadi Tutakuwa washindi.
3. Ukipungukiwa nguvu, Na vitani
Ukishindwa, Yesu atakutia Nguvu mpya
Ya Roho. Kwa nyimbo za shangwe kubwa
Utastahimili yote, Na kupata kuokoa
Wenye dhambi gizani.
Comments
Post a Comment