17 UKAE NAMI, GIZA LAFIKA

  1. Ukae nami, giza lafika! Usiniache, Mungu, Naomba! Unajua udhaifu wangu. Nakutegemea, Uwe nami!


  2. Maisha yangu mafupi sana. Uzuri wa dunia wapita. Kuna machozi na kufa pia. Mkombozi wangu, Uwe nami!


  3. Nakuhitaji wewe daima, Una uwezo wa kunilinda. Wewe shujaa wa kushinda wote, Kati’ hali zote, Uwe nami!


  4. Nionyeshe m-salaba wako, Nione nuru yako gizani. Na nikiishi, hata nikifa. Mkombozi wangu, Uwe nami!

Comments