170 NIKIZIONA SHIDA

1. Nikiziona shida Katika safari
Yesu anong'oneza Neno la faraja.
Anipa raha tele, Furaha na amani.
Naandamana naye Sasa na milele.


2. Na njia ikipita Juu ya milima,
Nakaribia mbingu, Nuru inang'aa.
Katika nuru hiyo naona kwa uwazi
Urithi wangu bora, Nchi ya ahadi.


3. Kwa imani naimba Hata hatarini,
Njia ikiwa ndefu, Nitavumilia.
Na nyota za ahadi Zinang'aa gizani,
Zaniongoza vema Nifike mbinguni.


4. Musa aliiona Nchi ya Kanani,
Kadhalika naona Nchi ya ahadi.
Kwa imani na heri Ninaishangilia.
Natamani kufika Kwa urithi wangu.


5. Nikiona mashaka Kwenye njia yangu,
Yesu aniongoza, Anichunga vema.
Ninaendelea tu, Mbinguni nifikapo
Nyimbo nitaziimba Za kumsifu Yesu.

Comments