171 MWENYEZI MUNGU NGOME KUU


1. Mwenyezi Mungu ngome kuu,
Silaha ya imara! Kwenye shida na huzuni
Twamtegemea sana. Mwovu akaribia
Kutia woga, Kujithibitisha Kwa njia ya hila,
Tusimwogope kamwe!


2. Nguvu zetu hazitoshi, Kwani
Twashindwa hima. Ila Mwenyezi yu nasi,
Twaambatana naye. Na jina lake huyo
Ni Yesu Kristo, Aliye Mshindi
Na mwenye mamlaka, Mfalme wa milele.


3. Na dunia ikijaa Na majeshi ya giza,
Tukiwa naye Mwenyezi, Hatutaona hofu.
Mwovu m-hukumiwa Hana nguvu, la,
Ya kutuharibu Maungo na roho;
Ashindwa na Mwenyezi


4. Maneno ya Mungu wetu, Tushikamane
Nayo, Hatufuati ya chini Twatafuta yaliyo
Juu, Tu hodari daima, Hata vitani,
Uzima twapata Kwake Mungu wetu;
Ufalme una Yeye.

Comments