1. Sisi kama viungo vya mwili wake Yesu
Mwokozi, Ruduma zetu tunazipenda
Tukisaidiana.
Tukisaidiana Kwa shangwe na umoja,
Kazi inaendelea mbele, Tukisaidiana.
2. Ikiwa vema kufanya kazi ya Yesu peke
Yangu, Tutafaulu tena zaidi,
Tukisaidiana.
3. Kama mchwa wanavyozijenga Nyumba
Za kichuguu, Nasi tuwe na juhudi ile
Kwa kazi yake Mungu.
4. Umoja wetu ni wa thamani,
Wampendeza Mungu. Anatubariki
Kwa neema Na kutufanikisha.
5. Bwana twaomba, katika Wewe,
Tuwe nao umoja! Kwa Roho wako
Utubatize, ili Tuwe na bidii!
Comments
Post a Comment