173 MAISHA KATIKA DUNIA


1. Maisha katika dunia Ni kupanda na
kuvuna, Apandaye katika mwili,
Atavuna hasara tu. Tukimtumikia
Mwokozi Tutapewa thawabu huko. Ni heri
kuishi na kufa Tukiwa watu wa Mungu.


2. Kwa neema kubwa kabisa Twakubaliwa
na Mungu. Kwa neema kubwa zaidi
Twapata kumtumikia. Kuishi kwa 'jili ya
Yesu Kati' yote ya dunia hii Na kuitangaza
Injili Ni faida kwetu kweli.


3. Wakristo watakapofika Mbinguni kumsifu
Yesu, Na mimi nataka kufika Kuimba
pamoja nao. Tutamshukuru Mwokozi
Aliyezichukua dhambi. Waliohudurnu
kwa pendo Watamsifu milele

Comments