1. Pendo kubwa la Babangu Linang'aa daima,
Walakini ana taka Na sisi tuwe nuru.
Nuru yetu iangaze Mbele ya watu wote,
Hata mtu mmoja mmoja Auone wokovu!
2. Dhambi zimetia giza Mioyoni mwa watu
Walakini watu wengi Waitafuta nuru.
3. Ndugu yangu angalia, Taa yako iwe safi!
Iwe nayo nuru kweli Ya kuwaangazia!
Comments
Post a Comment