1. Mungu akuita shambani mwake,
Nenda nawe pia umtumikie!
Ujitoe kweli kwa Mungu wetu,
Uhubiri Neno la Bwana Yesu.
Mtumikie! Mwokozi, Fanya kazi kwa
bidii! Nenda ukavune shambani mwake!
Wavuni wachache, Mavuno mengi.
2. Kumbuka jinsi Yesu apendavyo
Awatafuta waliopotea.
Nawe uwapende kwa pendo lake,
Naye atakupa baraka zake.
3. Uliyemwamini, Uende mbio Kwenye
Shamba lake. Usichelewe! Utumike vema
Omba kwa bidii, Na utapokea thawabu zake.
Comments
Post a Comment