178 YESU KUTOKA MBINGUNI


1. Yesu kutoka mbinguni Alifika huku
Nchi ya giza na dhambi, Ili tuokoke.


Nenda, nenda! Fanya kazi ya Yesu!
Yeye anakuhitaji Katika shamba lake!


2. Wanapotea gizani Ndugu zako wengi,
Nenda uwape habari: "Yesu aokoa!"


3. Nenda ukawahubiri Watu wa gizani.
Neno la Yesu Mwokozi Litawaokoa.

Comments