- Mungu wetu yu karibu, Kutupa nguvu
zake. Mbingu ina maghubari,
Tuletee mvua sasa.
Tusikie Mungu wetu, Tubariki saa hii!
Tunangoja, tunangoja, Kujazwa nguvu zako. - Mungu wetu yu karibu, Hapa patakatifu.
Sisi sote tunangoja, Kujazwa naye Mungu. - Mungu wetu yu karibu, Kwa imani
twaomba,“Tuwashie moto safi, Ndani ya
roho zetu!” - Mungu, ufungue mbingu, Twaomba nguvu
zako. Utubarikie sasa, Kwa rehema yako kuu!
Comments
Post a Comment