1. Bwana Yesu anatuuliza: "Nimtume nani
shambani?" Watu wenye dhambi wapotea,
Watolee Neno la Bwana!
''Ee Mungu, Ee Mungu! Uniguse sasa kwa makaa!
Ee Mungu, Sema tu! Mimi nipo hapa, nitume!"
2. Mtumishi wake Bwana Mungu Alisema:
“Mimi siwezi!” Aliposikia moto safi,
Akasema: “Nitume mimi!”
3. Mataifa mengi wanakufa, Hawamjui
Yesu Mwokozi. Twende kwao mbio,
Tuhubiri Neno la wokovu wa Yesu!
4. Siku za mavuno zitapita, Watenda kazi
Watarudi. Bwana wao atawapokea Na
Kuwakaribisha kwake.
Comments
Post a Comment