181 SISI TUTAZAME MBELE

1. Sisi tutazame mbele, Asubuhi yatujia.
Tumwamini Mungu wetu, Ataifanya kazi,
Kufukuza mashetani, Kuimiliki nchi.
Tutashinda tukiomba, Mungu atusikia.


2. Tarumbeta linalia, Tusikie mwito wake
Mungu wetu anataka tusimame imara,
Kila mtu awe safi Ndani ya moyo wake.
Tuache manung'uniko, Ili tupate nguvu!


3. Watu wake na tuimbe, Bwana Yu pamoja nasi!
Tutashinda majaribu Kwa uwezo wa Yesu.
Twende tumhudumie Kwa kumtolea mali,
Hata roho na akili, Zimtumikie Bwana.

Comments