184 NIENDE PALE


1. Niende pale penye giza na dhambi
Kuhubiri Neno la Mungu, Ili watu
Waliopotea njia Wafahamu pendo la Yesu.


Niende pale penye giza na dhambi,
Niwatangazie Injili, Ili wote wapewe
neema yake, Wapate kuona wokovu.


2. Bwana akinituma kwao wagumu,
Niachane na ndugu zangu, Hata wakiniita
Ni mpumbavu, Nitafanya anavyopenda.


3. Uliyeupoteza wakati wako, Katika mambo
Ya dunia, Amka wewe na uwaokoe wao,
Waliopotea dhambini.


4. Watu wengi wangali wamo gizani,
Wangoja kupata uhuru. Yesu ameniita,
Niende kwao Kuhubiri Neno la Mungu.

Comments