185 NI NEEMA KUBWA


1. Ni neema kubwa ya Mungu, Tumeitwa
kwa kazi yake, Kwenda kupanda
mbegu njema Katika roho za watu.


Nenda ukavune, Nenda ukavune! Sasa
mavuno tayari, Nenda ukavune!


2. Kama njia yako ni ndefu, Tegemea
Neno la Mungu. Bwana Yesu
Akuongoza, Unapopita jangwani.


3. Hata usipojulikana, Mtumikie Yesu
Vema, Naye anakuona wewe Na
Uaminifu wako.


4. Hata ukiwa huna nguvu, Nenda
Shambani mwake Mungu, Labda
Utaokota suke, Lililoachwa na ndugu.


5. Neno na nyimbo hazitoshi Kuwaamsha
Wenye dhambi, Bali mwenendo
Wako safi Utawavuta kwa Yesu.


6. Usichoke kupanda mbegu Kwa pendo
na matumaini! Ukipanda kwa shida
nyingi, Utavuna kwa shangwe kuu!


7. Na itakapokwisha kazi, Tutaitwa
kwenda mbinguni, Na tutawaona
wenzetu Waliovutwa kwa Yesu.

Comments