187 TU WAVUNAJI WA MUNGU


1. Tu wavunaji wa Mungu, Kwa Neno lake
Twaenda Shambani mwake kuvuna
Mavuno yaliyoiva. Kwa shangwe
Twayakusanya Na kuyaweka ghalani.
Tunamsifu Yesu aliyetukomboa kweli.


Twende shambani mwake Bwana atuita.
Mavuno yameiva, Muda unapita.
Siku zetu za kazi Zapita mbio mno.
Twendeni, Twendeni, Twendeni hima!


2. Tu wavunaji, twendeni, Tukayavune kwa bidii,
Tukusanye mavuno ya thamani ghalani mwake!
Yesu kwa upendo wake Awaita wapotevu.
Tukiacha suke dogo Ataona mara moja.


3. Wakati wetu ni mfupi. Twende tukafanye kazi!
Atutia uhodari na nguvu zake Mungu! Na
Usisimame bure Wavunaji ni wachache! Ee
Mvunaji wa Yesu, Mtumikie kwa bidii!

Comments