1. Wengi wasitasita Wanapoitwa na Bwana,
Lakini mwisho hukuta Wamechelewa kabisa.
Njoo leo, uje leo, Yesu anakuita, Njoo leo,
anakuita, Ee ndugu, usichelewe!
2. "Si leo", alisema Tajiri mmoja mjinga,
Na usiku alikufa, Akaenda hukumuni.
3. "Si leo", unasema Kwa Rafiki yako Yesu.
Ukumbuke neno lake "Leo siku ya wokovu."
4. "Si leo", ukumbuke Ndilo jibu la hatari,
Unaweza kupotea Usiingie mbinguni.
Comments
Post a Comment