190 KISIMA CHA LEHI


1. Kisima cha Lehi kingali Kinatoa
Maji yake. Na kila mtu mwenye kiu
Anakaribishwa kwake.


Maji safi Kisimani Hakitakauka milele.
Heri mimi, napumzika. Roho yangu inatulia.


2. Uliye na kiu rohoni, Ukilegea njiani,
Tazama kisima jangwani Chenye afya
Na uzima!


3. Mtungi ukiwa mtupu, Na ukikosa imani,
Tazama maji yamo tele Katika kisima
Hicho!


4. Na penye kisima cha Lehi Upange,
Upumzike! Uketi ukingoni mwake
Na moyo uburudishwe!

Comments