191 NIKASIKIA HODI


1. Nikasikia hodi, Mgeni a’fika,
Akiniomba: "Nifungulie!
:/:Umande umeshuka kichwani pangu
Na nywele zangu zimelowa maji.":/:


2. Si mgeni huyu, Ni Yesu Mwokozi,
Sauti yake nzuri na’jua.
:/:Ninamfungulia, Rafiki yangu;
Na siku hiyo sitaisahau:/:


3. Ananong'oneza rohoni: "U wangu."
Karibu naye ninatulia.
:/:Anitia nguvu na baraka tele,
Daima nitakaa kwake Yesu:/:


4. Kweli, mimi ni wa Mwokozi milele,
Ananiita "Ndugu, mpenzi",
:/:Ananikirimia hazina zake,
Ninaingoja siku ya arusi.:/:

Comments