192 NILISIKIA SAUTI


1. Nilisikia sauti ya Yesu: "Wajua
Niliyokufanyia? :/:Kwa ’jili yako
Niliteswa sana, Uje kwangu,
Kwani nakupenda!:/:


2. "Nilipokuwa huku duniani,
Nilivikwa taji ya miiba. :/:Na
Sikupambwa fedha na dhahabu,
Ila uchungu na majeraha.":/:


3. "Nilitundikwa pale msalabani,
Nilikufa kwa ajili yako,
:/:Tazama katika mikono yangu
Nimekuchora, ewe mwanangu.:/:


4. Haleluya, rohoni ninaimba,
Nimejiweka kwake Mwokozi.
:/:Na Yesu ananiongoza sasa,
Ili nifike huko mbinguni.:/:

Comments