193 NI NENO ZURI LA KUAMINI


1. Ni neno zuri la kuamini, Lastahili
kukubaliwa, Ya kwamba Yesu
Alitujia, Awaokoe wenye dhambi.


2. Kwa wenye dhambi, mimi wa kwanza,
Lakini nafurahi sasa, Sababu Yesu,
Mwokozi wangu, Alinisafisha kwa damu.


3. Mwokozi wetu yu nasi hapa, Atenda
kazi kati yetu. Awasha moto rohoni
mwetu. Nani aweza kumpinga?


4. Viziwi wanasikia sasa, Viwete
Wanaruka-ruka, Wenye ukoma
Watakasika, Injili inahubiriwa.


5. Ee Bwana Yesu, utuvuvie, Tujaze Roho
Mtakatifu! Twakuomba uwafungulie
Waliofungwa na Shetani.



6. Fungua mbingu, unyeshe mvua Mahali
pote penye jangwa! Upageuze,
pakachanue, Iwe furaha na shangwe kuu!


7. Na mataifa wakusujudu Mahali pa
utakatifu! Utukufu una Wewe Mungu,
Na sifa zote. Haleluya!

Comments