1. Umsikie Bwana Yesu Anayekuita leo!
Aliteswa, alikufa Kwa ’jili yako wewe.
Umsikie Bwana Yesu, Abisha mlangoni.
Umfungulie moyo. Sasa umpokee!
2. Siku zote ulicheza, Kupendeza mwili
wako. Ulimsahau Yesu Aliyekufilia.
3. Unasema: "Nitakuja Kusikia Neno lake! "
Ee rafiki, ukumbuke, Waweza kufa leo!
4. Yesu akuita leo Kwa neema na upendo.
Leo siku ya wokovu, Umfungulie moyo.
5. Tunampa Bwana Yesu Moyo na wakati wetu.
Yeye ni Mfalme wetu Milele na milele.
Comments
Post a Comment