195 TWASIKIA HABARI LEO


1. Twasikia habari leo, Yawaita watu wafike.
:/:Watu wa hapa na wa mbali,
Wote wapokee wokovu!:/:


2. Mtu wa dhambi, Njoo kwa Yesu. Yu tayari
kukuokoa. :/:Tena kwa nini wakawia?
Leo ni siku ya wokovu.:/:


3. Ulimkimbia Bwana Yesu, Aliyekufa msalabani.
:/:Usikimbie mbali tena,
Ila urudi kwa Mwokozi!:/:


4. Katika dhambi hutaona Amani kweli wala raha.
:/:Yesu mwenyewe atakupa
Raha halisi na furaha.:/:


5. Heri katika shida zote, Heri katika mambo yote.
:/:Ni hali ya mtu wa Mungu,
Kuwa na heri siku zote.:/:


Comments