1. Ndugu bila kujitahidi sana, Hutaingia mbinguni.
Neno la Mungu likae moyoni, Usije ukapotea!
Njia nyembamba na hata mlango, Ujitahidi kuingia
Humo! Ukubali leo wokovu wake, I1i ufike
Mbinguni!
2. Unapokutana na majaribu, Yanayoletwa na mwovu,
Uyashinde yote uyakutayo, Yaliyomo duniani!
Usiifuate kila sauti, Usije ukaipoteza roho!
Kwa ajili ya upendo wa Yesu Nakusihi jitahidi!
3. Bila imani hutaifikia Hiyo bandari ya mbingu
Wala kuupata uzima wake, Hilo ni neno la Mungu.
Kwa imani tu utaokolewa. Usikie sasa Neno la
Bwana! Tubu dhambi na umwamini Yesu!
Hiyo ni njia hakika.
4. Mungu awaita wote wafike, Waupokee uzima.
Atakupa nawe hazina zake, Ukizitafuta kweli.
Mungu Baba apenda roho yako. Yesu anapenda
kukuokoa. Roho Mtakatifu anakuita.
Heri kwako uitike!
Comments
Post a Comment