1. Hapo nilipokuwa dhambini, Niliumizwa
Rohoni. Sasa namsifu Yesu kwa shangwe
Kwani ameniokoa.
Ni neno kubwa la ajabu: Yesu aliniokoa
Naye anawapenda wote, Na atakuokoa!
2. Dhambi zote nilizozitenda Zimefutwa na
Mwokozi. Sikitiko kwa ’jili ya dhambi
Lilikomeshwa na Yesu.
3. Sasa mimi sitaki kurudi. Nachukia dhambi
Sana Nimeonja furaha ya Mungu,
Amani na raha yake.
Comments
Post a Comment