1. Ee mtu mwenye kiu, Ufike kwa Yesu
:/:Upate maji ya uzima, Usiwe na kiu
tena!:/:
Njoo kwa Yesu, Unywe maji hai!
Ufike na upewe uzima na nguvu!
2. Tazama ndugu wengi Wamekwisha
kunywa. :/:Ni heri kwamba maji hayo
Hayatakwisha kabisa.:/:
3. Unywe na wewe pia, Ukapate nguvu!
:/:Tumia katika shindano Upanga wa
Neno lake!:/:
4. Na mwendo wa imani Utakapokwisha,
:/:Na utakunywa maji ya uzima Kwa
Mungu milele.:/:
Comments
Post a Comment