199 NJONI WOTE MTESWAO

1. Njoni wote mteswao, Wote wenye huzuni
Kwa ajili ya makosa, Njoni sasa kwa Yesu!
Kwake mtaona raha, Upendo na amani.
Matulizo mioyoni Mtapata kwa Yesu.


2. Hakubali ulemewe na huzuni moyoni.
Yesu ni mchunga mwema, Akulinda zizini.
Pendo lake lina nguvu, Linaondoa woga.
Hufariji roho yako, Hukuleta kwa Mungu.


3. Yesu ndiye nyota yangu, Inayometameta.
Mtu amfuataye Ataiona njia. Hata nyota
za mbinguni Zikianguka zote, Nyota hiyo
ya milele Haizimiki kamwe.

Comments