20 BWANA YESU NIONGOZE

  1. Bwana Yesu niongoze, Salama baharini,
    Juu ya mawimbi mengi, Na katika dhoruba!
    Bwana Yesu niongoze, Ninakutegemea!


  2. Bwana Yesu, niongoze, Unitulize moyo!
    Sema neno moja tu, Patakuwa shwari kuu.
    Bwana Yesu niongoze, Unipe utulivu!


  3. Bwana Yesu, niongoze, Nishinde majaribu!
    Mengi yanidanganya, Na kunifumba macho!
    Bwana Yesu niongoze, Niwe mshindi kweli!


  4. Bwana Yesu, niongoze, Hata nivuke ng’ambo!
    Na nikiona giza, Nipe nuru na raha! Bwana
    Yesu niongoze, Uwe nami milele.

Comments