200 NJONI WOTE MLE MNYWE

1. “Njoni wote, mle mnywe!”
Yesu asema hivyo. “Nimetoa mwili
Wangu Kwa ajili ya wote.” Kila mwenye
Njaa na kiu Katika roho yake
Aje sasa kwake Yesu, aliyetufilia.


2. Ninakuja kwako Yesu,
Ukanithibitishe! Uliyekuwa maskini,
unipe utajiri! Nishibishwe mema yako
Na karama za Roho!
Unijaze Roho wako, Ulivyoniahidi!


3. Yesu ninakuja kwako,
Niungane na Wewe. Mimi mwenye
udhaifu,Ninakutegemea.Na kwa damu
yako,Yesu, Unitakase sasa! Nashiriki
mwili wako Na damu ya agano.


Comments