1. Njoo kwa Yesu Mwokozi,
Wewe nayeteswa!
Damu iliyomwagika Itakuosha moyo.
Njoo kwa Yesu mwokozi, Na atakuokoa!
Ulimwenguni ni dhiki. Kwake ni raha kweli.
2. Mbona kukawa dhambini, Bila uzima Wake?
Uje upesi kwa Yesu, Ili upate raha!
3. Saa zinapita upesi, Hazitarudi tena.
Bado kitambo kidogo Maisha yatakwisha.
4. Yesu atampeleka Bibi-arusi kwake.
Na tutaimba milele sifa za Mwana-Kondoo
Comments
Post a Comment