1. Yesu Mwokozi aita kwa pendo Mimi Pamoja nawe. Na yu tayari kuku-karibisha Wewe uliye mbali.
Urudi, urudi, Sasa urudi kwa Yesu!
Anakuita na anakungoja. Leo urudi kwake!
2. Usikawie anapokuita. Anakungoja,
Uje! Kuna nafasi karibu na Yesu.
Njia ni wazi kwako.
3. Nyakati zetu zapita upesi,
Hazitarudi tena. Njoo kwa Yesu,
Upate amani! Ipo nafasi leo.
4. Ona upendo mkubwa wa Yesu!
Unaenea pote. Na kwa neema
Anatukumbuka Wewe pamoja nami.
Comments
Post a Comment