1. Umgeukie Mwokozi Na ujitenge na dhambi!
:/:Babako angoja ufike Ili usiangamie!:/:
2. Kijana, unafurahia Anasa za ulimwengu.
:/:Baada ya muda kitambo Nawe utahukumiwa.:/:
3. Kwa nini kujiangamiza Kwa kufuata dunia.
:/:Usijipoteze dhambini Na kukosa tumaini.:/:
4. Umkimbilie Mwokozi, Naye atakupokea.
:/:Na utaokoka hakika Kwa nguvu ya damu yake!:/:
5. Walio mbinguni waimba, Wenye mavazi meupe.
:/:Hutaki kukaa pamoja Na watu wa Baba Mungu?:/:
6. Je, mwisho utaona wapi Mahali pa kujificha?
:/:Dunia itakapochomwa Utakosa kimbilio.:/:
7. Ujipatanishe na Mungu, Rafiki usichelewe!
:/:Ukimkataa Mwokozi, Utapotea milele.:/:
8. Chagua bila kukawia! Yesu atakupokea.
:/:Angoja ufike kutubu, Apate kukuokoa.:/:
Comments
Post a Comment