209 UWATAFUTE WANAOPOTEA

1. Uwatafute wanaopotea, Kwa pendo uwatoe
Dhambini! Lia pamoja na wenye huzuni.
Ukawalete kwake Mwokozi!


Waliopotea uwatafute! Yesu ni
Mwokozi hata kwao.


2. Na hata waliomwasi Mwokozi, Anawangoja
Warudi kwake. Uwafundishe kwa pendo na
Kweli. Awasamehe wakirejea.


3. Wengi wanasongwa na majaribu Ya kuficha
hamu ya wokovu. Uwaongoze kwa Yesu
Mwokozi, Wafahamishe pendo la Mungu!


Waokoe ni agizo la Bwana. Utapewa uwezo
Wa Mungu. Uwapeleke kwa Yesu Mpozi,
Wa huruma na afya kwa wote.


Comments