210 IMBA INJILI YA YESU

1. Imba Injili ya Yesu, Eleza uweza wake!
Lango la neema yake Ni wazi kwetu sote.


Imba, imba Injili, Na watu wasikilize,
Imba Injili ya Yesu, Maneno ya neema.


2. Imba Injili ya Yesu! Yawapa wote uhuru.
Imba habari ya damu Itakasayo moyo!


3. Imba Injili ya Yesu, Kwa wimbo uwafundishe!
Imba habari ya Yesu! Aweza kuokoa.


4. Imba Injili ya Yesu Iletayo tumaini!
Imba habari ya haki, Wamjue Mungu kweli!


5. Imba Injili ya Yesu, Hubiri amani kwao!
Na tumsifu Mwokozi! Afanya yote vema.


Comments