1. Njoo kwa Yesu, usisite! Akuonyeshe njia kweli.
Anakusihi, sikiliza: "Mtu wa dhambi, njoo!"
Heri, heri, tutakutana Kwake Mungu kwenye furaha!
Shida na shaka hazifiki Kwetu mbinguni juu.
2. Yesu aita: "Njoni wote!" Atatuliza mioyo yenu,
Kuwapa raha na upendo. Usikiaye njoo!
3. Sasa ni saa ya kuokoka. Uje upesi, umwamini!
Mwenye dhambi na sikitiko, Njoo kwa Yesu, njoo!
Comments
Post a Comment